Aliyekuwa mke wa Staa wa Muziki Ben Pol na mfanyabiashara kutoka Nchini Kenya Anerlisa ameonesha kutokupendezwa na komenti ya moja ya shabiki baada ya kumuita kuwa ni Tasa (Hana Uwezo wa Kupata Mtoto).
Kupitia instastory yake mrembo huyo alifunguka kuwa suala la kupata mtoto ni ndoto ya kila mwanamke.
"Kuna maoni mengi ambayo mimi hupuuza, lakini hii imekwenda mbali. Kwa kweli nimeguswa kwa sababu kuna wanawake tasa kweli katika ulimwengu huu. Nimesikitishwa kuwa mwanaume mzima anaweza kutoa maoni yake kuhusu mambo kama haya akijua ni wanawake wangapi wanahangaika siku baada ya siku kupata watoto,” Anerlisa alisema.