Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

TV

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Anerlisa afichua maelezo ya mkutano wake maalum na rais Ruto

Anerlisa Afichua Maelezo Ya Mkutano Wake Maalum Na Rais Ruto Anerlisa afichua maelezo ya mkutano wake maalum na rais Ruto

Thu, 13 Apr 2023 Chanzo: Radio Jambo

Mrithi wa Keroche, Anerlisa Muigai Karanja alikutana na Rais William Ruto katika Ikulu ya Nairobi siku ya Jumatano, Aprili 12.

Katika taarifa yake kwenye mtandao wa Instagram baada ya mkutano huo, mpenzi huyo wa zamani wa staa wa Bongo Ben Pol alisema alishangazwa sana na swali la kwanza ambalo rais alimuuliza wakati walipokutana.

Anerlisa alifichua kuwa mkuu huyo wa nchi alimpa changamoto kuhusu kwa nini hajawahi kujaribu kufanya biashara naye.

"Leo, nilikutana na Rais Dkt William Ruto. Swali lake la ufunguzi lilikuwa la mshangao kutoka moyoni; "Kwa nini haujajaribu kuniuzia maji yako?" Jinsi anavyoelewa mapambano ya mjasiriamali wa ndani ni jambo la kutia moyo. Na jibu ni wazi," alisema.

Binti huyo mkubwa wa seneta wa Nakuru, Tabitha Karanja, pia alitumia fursa hiyo kuishinikiza serikali ya Kitaifa na za kaunti kukumbatia bidhaa zilizotengenezewa hapa nchini kama njia ya kukuza bidhaa za ndani.

"Watendaji wa serikali lazima na wanapaswa kukumbatia "Bidhaa za Kenya" ili kuunga mkono kile ambacho Wakenya wanazalisha. Serikali ya Kenya na serikali za Kaunti lazima zitumie chapa za Kenya. Ni njia mojawapo ya kuwezesha chapa za humu nchini kukua," alisema.

Aliongeza, "Ninahisi heri kuwa tuna rais ambaye anapata hili.. Tujiandae kwa sura mpya."

Bi Anerlisa Muigai ni Mkurugenzi Mtendaji wa kampuni ya maji ya Nero Company Limited.

Mrithi huyo wa Keroche alianzisha kampuni hiyo mwaka wa 2015 na bidhaa yake ya kwanza ilikuwa ni maji ya chupa ya Executive.

Chanzo: Radio Jambo