Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Anerlisa: Ben Pol acha kunizungumzia, nina mengi mabaya kuhusu wewe

Anerlisa BENPOL Anerlisa na Ben Pol

Fri, 13 Jan 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Ni wazi kwamba @anerlisa hajafurahishwa na kitendo alichokifanya aliyekuwa mume wake, mwanamuziki Ben Pol baada ya kumzungumzia kwenye mahojiano yake na #AyoTv pia akisema kwamba hajawahi kufurahia maisha ya ndoa na bibie huyo raia wa Kenya.

Anerlisa amemtaka @iambenpol aache kumuongelea kwani na yeye ana mengi kumuhusu mkali huyo ama kuonyesha lakini amechagua kusimama kama mwanamke (kuwa kimya). Amehoji kwanini anapenda kumzungumzia ili yeye aonekane mbaya!

"Ben naona umenizoea na unachukulia ukimya wangu kama udhaifu wangu. Ulikuwa na uwezo wa kumwambia anaekuhoji asikuulize kuhusu mimi. Kwa nini unapenda kila mara mimi nionekane mbaya. Chini ya kapeti unanitumia jumbe tofauti tofauti na namna unavyoniongelea".

"Kama kweli wewe ni mwanaume, nakuomba uweke wazi jumbe zote ulizokuwa unanitumia tangu Desemba 25 hadi Januari 4, 2023. Nina mengi ya kuzungumza kuhusu wewe au kuonyesha, lakini nimechagua kusimama kama Mwanamke."

"Ni rahisi sana, acha kuniongelea," - ameeleza @anerlisa kupitia insta story yake.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live