Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Anachotumia Nandy kutengeneza Shepu yake chatajwa

NANDY Anachotumia Nandy kutengeneza Shepu yake chatajwa

Fri, 12 Jun 2020 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Kama unamfuatilia msanii Nandy "The African Princess" utagundua kuna mabadiliko katika mwili wake tofauti na mwanzo haswa kwenye shepu yake ya sasa ambayo imempa muonekano mzuri na kuvutia machoni mwa watu na wengine hutumia kusema amekuwa "amaizing"

Wengi wamekuwa wakijiuliza amekuwa anatumia nini ili kuwa na muonekano huo au labda amefanya surgery au kutumia vidonge, sasa majibu kamili kuhusiana na hilo amefafanua mpenzi wake Billnass kwenye show ya eNewz ya East Africa TV kwa kusema siri ya mabadiliko ni furaha tu.

"Nisingependa kumjibia ila yote ni maisha na mabadiliko ya mwili wa binaadam kama amekuwa, vitu vingi vimeongezeka na amekuwa na furaha sana nikimuona, kwa hiyo ni furaha tu ndiyo imeweza kubadilisha kila kitu sio suala la kutumia pesa nyingi hata kwa wanaomfahamu kwao wana asili ya miili"

Chanzo: www.tanzaniaweb.live