Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Anachotaka kufanya Harmonize si jambo la ajabu

73129 Wasafipic

Tue, 27 Aug 2019 Chanzo: mwananchi.co.tz

Dar es Salaam. Katika sanaa ya muziki duniani kote wasanii wengi wanakuwa chini ya lebo fulani lakini mwisho wa siku wanatoka katika lebo hizo kwa sababu mbalimbali.

Sababu hizo inaweza kuwa kuvunja mkataba, msanii kuhamia kwenye lebo nyingine, lakini wasanii wengine wanaamua kujisimamia wao wenyewe kutokana na mafanikio waliyopata kwenye lebo zao.

Kwa maana hiyo anachotaka kufanya msanii Harmonize kutaka kujiondoa kwenye lebo ya WCB ni jambo la kawaida kwa kuwa limeshafaywa na wasanii wengi duniani.

Wafuatao ni baadhi ya wasanii wakubwa waliowahi kujitoa kwenye lebo zao za awali na kuanzisha za kwao au kujiunga na nyingine.

Lebo ya Ogopa DJ’s ilianzishwa miaka ya 1990 jijini Nairobi nchini Kenya na ilipata umaarufu katika ukanda ya Afrika Mashariki kutokana na viwango vyake vya juu vya kutengeneza muziki.

Ogopa DJ’s ilisajili wasanii kama Ngoni, Rosemary Wahu maarufu kama Wahu aliyetamba na ngoma ya Niangalie, David Mathenge maarufu Nameless aliyetamba na kibao Nasinzia nikikuwaza, Longombas na Avirl.

Habari zinazohusiana na hii

Lakini baada ya wasanii Namless, Wahu pamoja na Avirl kupata mafanikio waliamua kuachana na lebo hiyo na kujiongoza wenyewe hadi hivi sasa wasanii Namless pamoja na Wahu ni maarufu na wanaendelea na maisha yao.

Mwanamuziki maarufu Tiwa Savage aliyekuwa chini la lebo ya Mavin Record ya Nigeria iliyoanzishwa na mtayarishaji wa muziki nchini humo Don Jazzy alijiondoa katika lebo hiyo mwaka 2019 baada ya kukaa miaka saba.

Tiwa Savage aliondoka katika lebo hiyo na kuamia lebo nyingine inayofahamika kwa jina la Univesral Music Group.

Nchini Marekani lebo ya Cash Money iliyoanzishwa na ndugu wawili Bryan Williums maarufu Baby na Ronald Williams maarufu Slim iliwasajili wasanii kama Lil Wayne, Drake na Nick Minaj, Bow Wow pamoja Dj Khaleed lakini wote mnajua walipo sasa hivi.

Mwaka 2015 Bow Wow aliamua kujitoa katika lebo hiyo na kuandika katika mtandao wake wa Facebook ameondoka katika lebo hiyo kwa Amani na kwamba yupo na bosi mpya Snoop Doggy Doggy pamoja na Jermaine Dupri. Alisema ameondoka kwa Amani kama anavyotaka kufanya Harmonize.

Mwaka huo huo 2015 DJ Khaled aliondoka katika lebo ya Cash Money na kusema ameondoka kwa amani pia katika lebo hiyo na atafanya kazi zake kwa kuniongoza mwenyewe. Leo wapenzi wa muziki wanajua jinsi Dj Khaleed anavyozidi kupata umaarufu.

Lily Wayne yeye alipoondoka Cash Money alianzisha lebo yake iitwayo Young Money lebo na kusaji wasanii kama Tyga ambaye hata hivyo alitoka katika lebo hiyo na kujiunga na lebo ya Good music inayomilikiwa na msanii Kanye West lakini mwishoni alianzisha lebo yake binafsi inayojulikana kama Last King.

Kutokana na kuwepo kwa mambo kama haya inaonyesha kuwa anachotaka kufanya Harmonize kilishawahi kufanywa na wasanii wengi tena wakubwa hivi sasa duniani.

Cha msingi ni jinsi alivyojipanga kujiendeleza kwa kuwa kuna wasanii wengine wanajiondoa kwenye lebo bila mipangilio na kuishia kupoteza umaarufu wao.

Chanzo: mwananchi.co.tz