Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Anachoimba Diamond hakieleweki?

Diamond Mtv Diamond Platnumz.

Mon, 6 May 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Inafikirisha sana pale wanapotajwa Wasanii wenye vipaji vikubwa huwa hatajwi sana Nassib wa Tandale, utasikia jamaa analazimisha anachoimba hakieleweki.

Watu wanasahau kazi ya Msanii ni kuburudisha na kuelimisha, ameshaelimisha sana kwenye Zuwena, Lala Salama, Mbagala na nyingine nyingi! Ameshaburudisha sana masikio ya Wapenda mziki, ni moja kati ya Wasanii wachache sana wenye uwezo wa kuelimisha na kuburudisha.

Ni moja kati ya Wasanii wachache sana ambao unaweza kuikataa ngoma yake mbele za Wanao halafu ukaenda kuimba bafuni peke yako, akiamua kuelimisha anamaanisha na akiamua kuburudisha anakera kabisa, amezaliwa kufanya hii kazi anayoifanya! Jitihada huzidi kipaji kama kipaji hakitofanya bidi, he is simply the best to grace the game.

Diamond wa Tandale akiamua anafanyaga mziki wowote, muda wowote kwa hadhira yoyote ile, unaweza usikubali kusikiliza mbele za watu ila hata bafuni utaucheza mziki wake, amezaliwa kufanya hiki anachokifanya as simple as that, hardwork beats talent when talent doesnt work hard.

Kimzaha mzaha anaweza kuufunga mwaka kwa hit ikiwa bado ni mwezi Mei. Kamfundisha Harmo kila kitu ila somo la kulazimisha ndio kitu ambacho Harmo hakushika vizuri, mwana akiamua asikilizwe yeye tu anaweza, promotion kali kama mziki kaanza leo ama hela ya mkopo ni njaa ya underground wa mkoani kabisa.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live