Lifestyle

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

SIL

Amwaga maji ya kwenye bwawa kutafuta simu

Rajesh Vishwas.png Amwaga maji ya kwenye bwawa kutafuta simu

Wed, 31 May 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Afisa mmoja nchini India Rajesh Vishwas, ametozwa faini ya zaidi ya dola 640, kwa kutiririsha lita za maji kutoka kwenye bwawa la Kherkatta lililopo jimbo la Chhattisgarh nchini humo, kutafuta simu yake aliyoidondosha wakati akijipiga 'selfie'

Afisa huyo ambaye ni Mkaguzi wa chakula, alijichukulia maamuzi hayo bila kupata kibali kutoka kwa mamlaka, na alidai amefanya hivyo kwa simu hiyo ilikuwa na data muhimu za serikali.

Lakini Rajesh anasema awali alipiga mbizi, Baada ya wapiga mbizi katika eneo hilo lakini hakufanikiwa kuiona simu, ndipo alilipia pampu ya dizeli kuletwa.

Pampu hiyo ilivuta maji ya bwawa hilo kwa kwa siku kadhaa, ikitoa maelfu ya lita za maji, lakini wakati simu ilipopatikana, ilikuwa haiwezi tena kufanya kazi.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live