Lifestyle

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

TV

Nchi

Kijamii

SIL

Ampeleka mchumba wake Mahakamani kisa kakataa kumuoa

NDWAAAAAAAAAA Ampeleka mchumba wake Mahakamani kisa kakataa kumuoa

Thu, 10 Dec 2020 Chanzo: millardayo.com

Mwanamke mmoja aliyefahamika kwa jina la Getrude Ngoma (26) wa mjini Ndola nchini Zambia, amempeleka mchumba wake mahakamani kwa kushindwa kumuoa baada ya kuwa naye kwenye mahusiano kwa muda wa miaka nane tena akiwa amemzalisha mtoto.

Getrude amesema amechoka kumvumilia mwanaume huyo aliyefahamika kwa majina ya Herbert Salaliki ambaye alimuahidi kumuoa na badala yake hajafanya hivyo kwa kisingizio cha kutomudu gharama za harusi wakati tayari amekwisha toa mahari.

Jaji Evelyn Nalwize ambaye ameisikiliza kesi hiyo katika Mahakama ya Jimbo la Kabushi, Ndola alimshauri Getrude kumaliza madai ya tofauti zao nje ya mahakama.

Chanzo: millardayo.com