Mwanamama Rachel Bailey wa Florida, Marekani ameweka wazi kumnyonyesha maziwa mumewe Alexander ili kuimarisha ndoa/mahusiano yao zaidi.
Mama huyo wa watoto watatu anasema ameanza kumnyonyesha mumewe tangu mwaka 2017 jambo ambalo limefanya kuwa pamoja na karibu zaidi kama wanandoa.
"Hii sio utani kwetu, alianza kunisaidia kipindi nasikia maumivu kwenye matiti baadaye ikawa kihisia. Tangu ameanza kunywa ngozi yake imekuwa nzuri na anapenda kunywa maziwa yangu kuliko ya Ng'ombe" amesema Rachel
Pia ameongeza kusema huwa anamnyonyesha maziwa mara 3 mpaka 4 kwa siku.
Una lipi la kumwambia Rachel? Tupe maoni yako