Lifestyle

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

SIL

Amnunia mke wake kwa miaka 20 baada ya kumkera

Miaka 20 Amnunia mke wake kwa miaka 20 baada ya kumkera

Tue, 29 Aug 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Hivi mpenzi wako akikuudhi huwa unachukua uamuzi gani kama adhabu kwake? Sasa ukisikia kuwa uyaone sio maghorofa, huku mtandaoni kuna huyu mwanaume aliyetambulika kwa jina la 'Otou Katayama' ambaye mnamo mwaka 2017, alikiri kwamba hakuwai kuzungumza na mkewe kwa miaka 20, licha ya kuishi pamoja huko Nara, Japan.

Mtoto wao wa kiume mwenye umri wa miaka 18, Yoshiki, alifunguka kwamba Bwana Otou, alikuwa akiwasiliana na mkewe kwa njia ya kutikisa kichwa na miguno tu.

Mtoto wao huyo wa kiume alianzisha mipango ya kuwakutanisha kiujanja ili wazungumze tena kwa kuongea kwa sauti kama ilivyokuwa zamani na alifanya mkutano kati ya wanandoa hao kwenye bustani ambapo awali wanandoa hao walipatumia kuchumbiana kwa mara ya kwanza na hapo ndipo Otou alifunguka ya moyoni kuhusu wivu wake dhidi ya uangalizi wa mke wake kwa watoto wao.

Mazungumzo haya yaliyobeba hisia nzito kwenye mioyo ya wote wawili, sio siri yalionesha mengi yaliyokua yamejificha kwenye nafsi zao ikiwa ni mara yao ya kwanza kuongea tena baada kuwa kwenye ndoa iliyotawala ukimya mwingi kwa miaka mingi.

Una maoni gani juu ya historia hii ya mapenzi?

Chanzo: www.tanzaniaweb.live