Lifestyle

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

SIL

Amkimbia mpenzi wake baada ya kugundua ana ujauzito wa mapacha watatu

Ujauzito 1 1024x576 Amkimbia mpenzi wake baada ya kugundua ana ujazito wa mapacha

Fri, 25 Aug 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mwanamke mmoja kutoka nchini Nigeria mwenye umri wa miaka 27 anayetambulika kwa jina la Marry, adai kukimbiwa na mpenzi wake baada ya kumwambia kuwa anaujauzito na anatarajia kupata watoto watatu.

Mwanamke huyo amefunguka kuhusu masaibu hayo anasema walipanga kufunga ndoa na mpenzi wake huyo kabla ya kuondoka kisa ujauzito wa watoto watatu.

Aliendelea kueleza kuwa mwanaume huyo alienda kuwaona wazazi wake kwa ajili ya kuomba ruhusa ya kumuoa Marry lakini baada ya kumpa ujauzito alitokomea mahali pasipo julikana .

Sasa akiwa na watoto hao wachanga watatu, Mary amedai yeye na wanawe wanaishi kwa huruma ya mwenyenyumba.

Alifichua kuwa awali alifanya kazi ya kushona nguo lakini ujauzito ulimfanya adhoofike, na alishindwa kuendelea na shughuli hiyo.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live