Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Amini: Mtoto wa Linah sio wa kwangu

Amini Linah Amini na Linah.

Thu, 18 Apr 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Staa wa kitambo wa Bongo Fleva kutoka Jumba la Vipaji (THT), Amini Mwinyimkuu 'Amini' amefunguka kwamba tetesi za mitaani kwamba yeye ndiye baba wa mtoto wa staa mwenzake, Linah hazina ukweli wowote.

Amini ambaye aliwahi kuwa kwenye uhusiano wa kimapenzi na Linah kisha kumwagana na baadaye kurudiana amekanusha madai hayo ambayo yamekuwa yakisemwa na baadhi ya mashabiki kuwa mtoto yule ni wake.

“Mtoto keshakuwa yule, mimi sifanani naye sema mwamba aliyezaa naye ana rangi kama ya kwangu. Hata nywele sijafanana na yule mtoto, hata kucha,” amesema Amini.

Amini aliwahi kunukuliwa akisema kuwa kama kuna kitu ambacho anakitamani zaidi ni kumpachika mimba mpenzi wake huyo ili tu roho yake itulie kitu ambacho anakiomba sana kwa Mungu, kitokee na anaamini kwa mapenzi yake kitatimia.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live