Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Amber Rutty na mumewe waa-update ndoa yao

AMBER Amber Rutty na mumewe waa-update ndoa yao

Sun, 21 Jun 2020 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Msanii Amber Rutty ame-update ndoa yake na mumewe Davil baada ya kuachana kwa muda mrefu kisha kutalakiana kwa talaka iliyodumu kwa muda wa miezi miwili na nusu.

Akizungumza na EATV & EA Radio Digital Amber Rutty amesema wameamua ku-update ndoa na mahusiano yao kwa sababu kulitokea malumbano na walishindwa kuelewana na sasa hivi wamerudiana tena.

"Siku ya jana tulikuwa tuna update mahusiano yetu tangu tulivyofunga ndoa hapo katikati kulitokea malumbano, kushindwana kuelewana na tukafarakana ila sasa tumerudiana, kwa hiyo mume wangu ameamua kua-update kwa kusheherekea ili mahusiano yetu yawe mapya kabisa na alinifanyia suprise ya kunivalisha pete" amesema Amber Rutty

Chanzo: www.tanzaniaweb.live