Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Amber Lulu atangaza kuolewa hivi karibuni

Lulu Amber Amber Lulu

Thu, 3 Nov 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mwanamuziki Amber Lulu ametangaza hatua nyingine katika uhusiano wake na mpenzi wake.

Katika Instastory zake, Lulu alisema kuwa ataolewa hivi karibuni na kwamba halikuwa jambo ambalo alidhani litatokea. "Naolewa. Asante Mungu, sijatarajia hili," Lulu alisema.

Hivi majuzi, mwanamuziki huyo alikuwa amedaiwa kuwa kwenye mahusiano na jamaa fulani.

Hii ni baada ya Amber Lulu kupakia picha ya kimahaba akiwa na msanii wa Bongo Fleva The Dream na kunogesha tetesi za kuwa kwa sasa moyo wake umetulia kwa msanii huyo ambaye kwa muonekano ni mdogo kiumri zaidi yake.

Kabla ya hayo msanii huyo alikuwa amepakia picha yake na kudokeza kwamba alikuwa amepata mpenzi anayempenda mwanawe.

Lulu alisema jinsi alivyokuwa akipitia ukatili kutoka kwa mume wake wa awali licha ya kumuonyesha mapenzi.

"Kwako nimepumzika nimechoka vipigo dharau nampenda unavyo tupenda mimi na mwanangu @arianna_the_brand tunakupenda sanaa."

Hata hivyo, msanii huyo hakufichua sura ya mpenzi wake na kuwaacha mashabiki wakitaka kujua ni nani.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live