Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Amber Lulu achafua hali ya hewa

Amber Lulu Na Mpenzi Wake Amber Lulu achafua hali ya hewa

Fri, 30 Sep 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Amber Lulu; ni mwanamama anayekiwasha kunako Bongo Fleva ambaye amechafua hali ya hewa baada ya kusema la moyoni kuhusu ishu ya yeye kama anaweza kudumu kwenye uhusiano wa kimapenzi na mwanaume asiyekuwa na pesa za kutosha.

Amber Lulu amesema; “Siwezi kuwa na mahusiano na mwanaume asiyekuwa na pesa.

“Mimi ninahitaji kutunzwa na pia matunzo yangu yanahitaji pesa sana, sasa nitawezaje kudumu na mwanaume asiyekuwa na pesa?”

Ishu hiyo imesababisha Amber Lulu kushambuliwa na baadhi ya wanawake wenzake wakimtaka kutafuta pesa yake na kamwe asitegemee pesa za mwanaume.

Taarifa za ndani zinadai kwamba, Amber Lulu na baba wa mtoto wake aitwaye Emba Botion ambaye wamejaaliwa mtoto mmoja wa kike aitwaye Ariana, wameshaachana na chanzo ni mambo hayohayo ya jamaa kutokuwa na pesa hivyo mwanamama huyo akidai kuwa alikuwa mzigo kwake.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live