Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Amanda Poshy achafukwa

Amanda Poshy Amanda Poshy achafukwa

Wed, 13 Dec 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Kufuatia matukio ya watu wanaojiua na wengine wakifa na siri za maumivu yao mioyoni mwao, Amanda Poshy mwigizaji wa Kibongo anayeishi Uingereza kwa sasa na familia yake, afunguka ikiwemo kisa chake yeye.

"Wapendwa kila siku naandika mnaweza kuona mimi sina kazi lakini kwenye kuelekezana naokoa maisha ya watu wengi bila kujua na pia siwezi kushangaa Waafrika asilimia 90% tumejaa chuki, kudhalilishana, dharau, ushenzi hata mtu ana jambo lake anaogopa kukuambia na yote hii inafikia mtu anabeba mazito mpaka kifua kinajaa kinakaribia kupasuka anaona suluhisho bora kujitoa uhai.

"Ukiangalia matukio ya baadhi wanaojiua kuna wapuuzi wasio na akili wanatukana wanaojiua wanawasema vibaya lakini narudia tena unaloweza kulibeba wewe kuna mwenzio hawezi na analoweza kulibeba mwi ngine wewe huliwezi.

"Nawapeni mfano wangu mimi kidogo tu, kwenye maisha yangu nimepitia maumivu makali mno kiasi kuna mambo nimeyapitia ambayo hata bibi na babu zangu hawajayapitia kuna kipindi nilikata tamaa na ukiangalia unaweza ukamueleza mtu akachukulia kama vile ni kitu cha kawaida ila mtu huyo huyo angesikia nimejiondoa uhai angesema khee kumbe alikuwa na mazito.

"Lakini huwezi amini nilikutana na mkaka kwenye park alinikuta nalia yule kaka aliniomba nimuambie nini tatizo hamuwezi amini maneno aliyoniambia nilisimama nikajifuta machozi tokea siku ile nilijiona mpya.

"So hii ndio maana ya kila wakati kuwaambia kama una tatizo nitumie Dm nieleze angalau ushauri tutakaopeana huwezi jua utakusaidia kiasi gani au pia ni bora usimamishe mtu barabarani mweleze kinachokuumiza usiogope.

"Halafu niwape siri hakuna watu wazuri wa kuongea nao kama watu msiofahamiana na wengine inakuwa ni malaika waliokujia kwa njia tofauti," ameandika

Chanzo: www.tanzaniaweb.live