Lifestyle

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

SIL

Alvaro Morata aachana na mkewe

Alvaro Morata Sdss Alvaro Morata

Tue, 10 Sep 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Nahodha wa timu ya taifa ya Hispania, Alvaro Morata amechana na mke wake, Alice Campello kutokana na mrembo huyo kuwakataa wazazi wa Morata wasishuke jukwaani kusherehekea ubingwa wa UEFA EURO 2024 dhidi ya England nchini Ujerumani.

England na Hispania zilifanikiwa kutinga fainali ya michuano hiyo na mchezo ulipigwa Julai 14 nchini Ujerumani ambapo Hispania ilifanikiwa kutwaa ubingwa baada ya kushinda mabao 2-1.

Morata na mkewe wakaja kuachana mwezi Agosti kwa madai kwamba ugomvi wao ulianzia katikati ya uwanja wakiwa wanasherehekea ushindi huo.

Alice alimwambia Morata kuwa angependa kushuka katikati ya uwanja kutoka jukwaani akiwa yeye, watoto na rafiki wa mrembo huo, lakini hataki kuwaona wazazi wa Morata wakishuka uwanjani, ila wabaki jukwaani.

Mgogoro huo ukawa mkubwa huku Morata akitaka kujua kwanini wazazi wake wasije kusherehekea ubingwa huo pamoja? Akaona isiwe tabu, tuachane wazazi ni muhimu. Wawili hao walikuwa kwenye ndoa kwa kipindi cha miaka saba na kufanikiwa kupata watoto wanne.

Unadhani Morata amefanya maamuzi sahihi?

Chanzo: www.tanzaniaweb.live