Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

TV

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Aliyoyapitia mke wa Prof. Jay anastahili kuwa mwanamke shupavu

Professor Jay, Mkewe Washerehekea Maisha Na Afya Aliyoyapitia mke wa Prof. Jay anastahili kuwa mwanamke shupavu

Tue, 12 Sep 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mitihani ameumbiwa Binadamu, kuna mitihani mikubwa ya kati na mitihani midogo, mitihani haina tofauti na kujaribiwa. Kuna kujaribiwa na Mungu lakini pia kuna kujaribiwa na Shetani, jaribu la Shetani ni rahisi kulishinda kwasababu linakuja na vinono/starehe.

Jaribu la Mungu ni gumu kulishinda kwasababu linakuja na kaugumu flani ambako kwa kawaida siyo rahisi kushinda, ndiyo maana Shetani ana wafuasi wengi.

Mwaka mmoja kama siyo miwili nyuma dunia ilishuhudia tukio la kusikitisha, tukio lililoitetemesha mioyo ya watu wengi ni baada ya kutoka kwa taarifa kwamba msanii wa Muziki wa Bongo Fleva Professor Jay alikuwa anaumwa hoi bini taabani, maombi yalikuwa mengi, maneno yalikuwa mengi mazuri na mabaya, watu wabaya na wazuri walijiinua wakaonekana, lakini hofu kubwa ilikuja baada ya Mange Kimambi kuvujisha picha tata zilizomuonyesha Professor Jay akiwa katika chumba maalumu cha ICU akipambania uhai wake.

Mange hakuishia kuposti picha tu, picha hizo ziliambatana na ujumbe ambao haukuwa na maneno mazuri, alitabiri mwisho wa Professor Jay, na akaongeza kuwa ikiwa atapona hatakuwa mzima atapooza.

Kimsingi hayakuwa maneno mazuri, yalikuwa ni maneno ya aibu, fedheha, uzalilishaji na zaidi yaliwavunja moyo watu wengi, wengi walionyesha kuumia.

Lakini kwa muda wote huo, Mke wa Professor Jay ambaye ndiye alikuwa mtu wa kwanza wa karibu wa Professor Jay kipindi anaumwa taabani hakuwahi kutoa neno lolote, alionyesha ujasiri na ushupavu. Fikiria ikiwa wewe ambaye ni shabiki tu uliumizwa na maneno ya Mange na watu wengine vipi kuhusu mke wake?

Mke ambaye wanaishi kama ndugu. Haikuwa rahisi! na haikuchukuwa muda mchache mpaka Professor Jay kukaa sawa lakini mwanamama huyo alivumilia, alipambana na Shetani hadi kumshinda ilitumika nguvu ya ziada ya kiimani.

Tumeshuhudia wanawake na hata wanaume wengi huwa wanawaacha wenza wao pindi wanapopatwa na tatizo kama alilopata Professor! wengi wao huwa wanazikimbia ndoa zao lakini kwa mke wa Professor haikuwa hivyo, hakujibu maneno ya watu aliwaacha wajibiwe na Mungu kwamba hapangi mwanadamu isipokuwa Mungu.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live