Lifestyle

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

SIL

Aliyepotelea baharini siku 438 akila samaki wabichi na kasa

Jose Salvador Alvarenga José Salvador Alvarenga.

Fri, 22 Mar 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Hakuna aliyeamini kwamba binadamu huyu angekuwa hai baada ya kupotea baharini kwa takribani miezi 14 na kutafutwa bila mafanikio, lakini ajabu mtu huyu aliishi kwa siku 438 baharini mlo wake ukiwa samaki wabichi na kasa.

José Salvador Alvarenga ambaye ni mvuvi raia wa Amerika mwaka 2012 alipotelea Baharini akiwa ameenda kuvua samaki na rafiki yake wa uvuvi karibu na Mexico kwenye bahari ya Pacific na kukutana na dhoruba kali iliyopelekea chombo chao kwenda mrama na kupoteza uelekeo baharini.

Mvuvi mwenzake alifariki baada ya miezi miwili na nusu, na kumwacha Alvarenga peke yake katika bahari ya Pacific akitapatapa, alikaa bila msaada wa vikosi vya uokozi vilivyokuwa vikimtafuta bila mafanikio kwa muda wa siku 438.

José baada ya kuokolewa alieleza kuwa kwa muda wote huo alikuwa anaishi kwa kula samaki wabichi na kula kasa wabichi baada ya kupelekwa na mawimbi makali umbali wa zaid ya Km 8000 mbali na kingo za bahari.

Kisa chake kimekuwa cha kusisimua sana kwani ni zaidi ya mabaharia milioni mbili wanakadiriwa kufa wakati wa safari za umbali mrefu bahari ya Pasific kati ya miaka ya 1500 na 1800.Lakini mwamba huyu alitoka akiwa hai isipokuwa akiwa na upungufu wa maji mwilini.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live