Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Aliyemuua Nipsey Hussle ahukumiwa jela miaka 60

Nipsey Hussle Jm Aliyemuua Nipsey Hussle ahukumiwa jela miaka 60

Thu, 23 Feb 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mshitakiwa Eric R. Holder, Jr. amekutwa na hatia ya kufanya mauaji ya mwanamuziki ambaye jina lake halisi ni Ermias Asghedom 'Nipsey Hussle' tukio lililotokea mwaka 2019, Los Angeles nchini Marekani.

Hussle alikuwa baba wa watoto wawili aliowapata na nyita wa filamu, Lauren London, aliuawa akiwa na umri wa miaka 33 katika tukio ambalo pia liliwajeruhi watu wawili.

Holder ambaye alimuua Nipsey kwa kumpiga risasi 10, pia amekutwa na makosa mengine mawili ya kujaribu kuua bila kukusudia watu wawili waliojeruhiwa kwa risasi.

Akiwa Mahakamani mtuhumiwa hakuonesha mshtuko au ishara yoyote baada ya Jaji kusoma hukumu yake licha ya kuwa wakili wake ameahidi kukata rufaa.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live