Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Aliyefuta Enjoy ya Jux na Diamond naye akutwa na majanga

Sapolog Aliyefuta Enjoy ya Jux na Diamond naye akutwa na majanga

Wed, 16 Aug 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Msanii kutoka Congo anayefahamika kwa jina la Issas Joana (22), maarufu kama Sapologuano Odenumz, ambaye ameifuta audio ya Enjoy ya Juma Jux ft Diamond Platnumz na yeye yamekuta majanga.

Sapologuano alidai kuwa ameufuta wimbo huo kwa sababu wame-copy ngoma yake yake ya 'I Found Love', sasa wimbo huo huo wa ‘I Found Love’, umepigwa copyright na kampuni ya muziki ya AfriCori ya nchini Afrika Kusini.

Sapologuano amekiri kuwa ni kweli wimbo wake umepigwa copyright saa 5 baada ya yeye kuupiga copyright wimbo wa Enjoy.

Msanii huyo amedai kuwa kampuni hiyo ndio inasimamia kazi za Jux, hivyo aliombwa na YouTube kuthibitisha kama kweli wimbo wake umenakiliwa. Amesema tayari ameshatuma taarifa zote na sasa anasubiria majibu.

Msanii huyo ameenda mbali zaidi na kueleza kuwa iwapo hawatamalizana naye ndani ya siku mbili basi wajiandae kwa pigo jingine takatifu kwani ataifuta hata video ya wimbo huo.

Sapologuano ameweka wazi kuwa siku kadhaa nyuma aliwahi kumtumia Jux ili wafanye kazi lakini msanii huyo alimzungusha na amekuja kuisikia Melody yake kwenye wimbo wa Jux na Diamond #Enjoy.

Aidha, Sapologuano ameongeza kuwa hivi karibuni alimtafuta Jux ili wazungumze na waone namna ya kulimaliza suala hilo lakini staa huyo wa Bongo Fleva alimkaushia jambo lililomfanya kuamua kuifuta YouTube.

Nini maoni yako?

Chanzo: www.tanzaniaweb.live