Lifestyle

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

SIL

Alikosa malezi ya binadamu akalelewa na mbwa mwitu

Dina Sanichar Dina Sanichar.

Mon, 19 Feb 2024 Chanzo: indiatimes.com

Dina Sanichar ni mwanadamu ambaye alipitia wakati ngumu sana katika maisha yake kwani hakuwahi kabisa kupata malezi ya mama na baba akiwa mtoto bali alipata malezi kutoka kwa mbwa mwitu.

Dina Sanichar inadaiwa alizaliwa mwaka 1860 nchini India, mwaka 1867 wawindaji wakiwa kwenye Shughuli zao Bulandshahr, Uttar Pradesh, India walimuona mtoto mdogo kwenye mapango akiwa amechanganyika na kundi kubwa la Mbwa mwitu.

Wawindaji hao walimchukua mtoto huyo akiwa na umri wa miaka 6 kisha wakampeleka kwenye kituo cha watoto yatima, baada ya kufika kituoni hapo mtoto alipewa jina la "Sanichar" kwa kiingereza ikimaanisha "Saturday" kwa sababu aliwasili kituoni hapo siku ya jumamosi.

Baada ya kufika kituoni hapo Dina Sanichar alikuwa hawezi kujichanganya na watu, alikuwa anatembea kwa miguu minne, Chakula chake kilikuwa ni nyama mbichi pia alikuwa hawezi kuongea zaidi ya kutoa sauti kama mbwa mwitu.

Baada ya kuishi na binadamu kwa zaidi ya miaka 20 Dina Sanichar aliweza kutembea kwa miguu miwili lakini hakuweza kuongea maisha yake yote.

Mwaka 1895 Dina Sanichar akiwa na umri wa miaka 34 alifariki kwa ugonjwa wa TB, inadaiwa alikuwa anavuta sana sigara.

Mpaka leo hii haijafahamika kwanini Wazazi wa Dina Sanichar walimtelekeza mtoto huyo mpaka akakutana na mbwa mwitu wakamlea.

Chanzo: indiatimes.com