Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Alikiba na Amina washerehekea 'birthday' ya mtoto wao

Alikiba Aminaz Alikiba na Amina washerehekea 'birthday' ya mtoto wao

Wed, 21 Feb 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Siku ya Jumatatu, staa wa Bongo, Ali Saleh Kiba almaarufu Alikiba na aliyekuwa mke wake Amina Khalef walimsherehekea mtoto wao Keeyan Alikiba mnamo siku yake ya kuzaliwa.

Keeyan ambaye ni mtoto wa kwanza wa Alikiba na mrembo huyo wa Kenya aliadhimisha siku yake ya kuzaliwa ya tano mnamo Februari 19 na wazazi wenza hao wawili walikuwa na ujumbe mzuri kwake.

Kwa upande wake, bosi huyo wa King's Music Records alishiriki picha nzuri ya mvulana huyo na kumtakia siku njema ya kuzaliwa.

“Kheri ya siku ya kuzaliwa mwanangu,” Alikiba aliandika.

Bi Amina Khalef pia alishiriki picha sawa na kuomba baraka za Mungu kwa mwanawe.

“Baraka za Mungu na ziwe nawe sikuzote,” aliandika.

Alikiba na mkewe huyo wa zamani kutoka Kenya walikuwa wamejaliwa watoto wawili kabla ya ndoa yao kugonga mwamba takriban miaka miwili iliyopita.

Talaka ya staa huyo wa bongo fleva na Bi Amina Khalef iligonga vichwa vya habari mnamo mwezi Februari mwaka wa 2022

Ombi la talaka liliwasilishwa mahakamani na mwanamke huyo mzaliwa wa Pwani ya Kenya na kusikilizwa kwa miezi kadhaa kabla ya kuamuliwa.

Miezi kadhaa baadaye, mama huyo wa watoto wawili alitangaza kuwa yupo 'huru rasmi', ujumbe ambao ulieleweka kumaanisha kesi ilikuwa imekamilika.

Amina, ambaye sio maarufu sana kwenye mitandao ya kijamii, alipakia picha ya ngome iliyo wazi na ndege akiruka.

Pia alifuta picha zote na AliKiba, zikiwemo zile za harusi yao ya kifahari iliyofanyika mnamo Aprili 2018.

Duru za kuaminika sasa zilisema AliKiba alijaribu kuokoa ndoa yake, ingawa mwishowe juhudi zake zikaambulia patupu.

“Tangu alipoomba talaka, Alikiba amesafiri kwenda Kenya mara nyingi akiwa hajitambui ili kujaribu kurekebisha mambo, lakini Amina alionekana kuwa ameamua,” chanzo cha habari kilisema.

Kabla ya kudai talaka, inasemekana Amina alimpa mwimbaji huyo nafasi ya kurekebisha mambo, lakini hakufanya hivyo.

"Amina alikuwa ameamua kutulia na kulea familia na Ali," chanzo kilisema.

"Ilifika wakati alihisi kuwa alikuwa akimchukulia kawaida na hakuweza kuvumilia tena. Aliamua kuondoka."

Chanzo: www.tanzaniaweb.live