Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Alikiba kufanya shoo 10 Marekani

Ali Kiba Alikiba

Thu, 25 Aug 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Star wa Bongofleva, Alikiba anatarajia kufanya shoo 10 nchini Marekani kupitia ziara yake, Only One King US Tour 2022 itakayoanza Septemba 2 huko Houston.

Ni zaidi ya miaka minne Alikiba hajafanya tour nchini humo na sasa anareja kwa ajili ya kuitangaza albamu yake ya tatu, Only One King iliyotoka rasmi Oktoba 4, 2021.

Tour hiyo itakayomalizika Oktoba Mosi itafanyika maeneo kama Houston, Minneapolis, Phoenix, Des Moines, Atalanta, Lexington, Manchester, Chicago na Dallas.

Ikumbukwe Alikiba anareja Marekani ikiwa ni mara ya kwanza tangu rafiki yake, R Kelly kuhukumiwa kifungo cha miaka 30 jela, Kiba na Kelly walifanya pamoja ngoma, Hands Across The World katika mradi wa One8.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live