Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

TV

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Alikiba atupa jiwe gizani chati ya Sallam, Tale

Image 257.png Alikiba atupa jiwe gizani chati ya Sallam, Tale

Tue, 27 Dec 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mwimbaji wa Bongo Fleva, Ali Saleh Kiba ‘Ali Kiba’ ametupa jiwe gizani, kwa watu ambao amedai kuwa wanajaribu kutumia majina ya wasanii wengine likiwamo jina lake, ili kufanikisha mambo yao kibiashara.

Kupitia ukurasa wake wa mtandao wa Instagram, Ali Kiba ameweka ujumbe wenye kudhihirisha kuchukizwa kwake na mpango ambao amebaini kuwa umetengenezwa kwa dhamira ya kuwashusha baadhi ya wasanii, ukitumika kufanikisha maambo yao binafsi.

Licha ya kutokuwataja kwa majina waliomkera, Kiba ameandika ujumbe wenye maelekezo yenye kuashiria kutoridhishwa na chati ya muziki iliyotolewa na mameneja wawili wa msanii Diamond Platnumz, Sallam Sk na Babu Tale, iliyojumuisha jina lake kama miongoni mwa wasanii wao pendwa waliofanya vyema kwa mwaka 2022.

Amesema, huo ni mpango wa kutafuta choko choko ili kuibua zogo kwa kusudio la kufanikikisha tukio la show yao inayotarajiwa kufanyika mwishoni mwa mwaka huu huku akiongeza “I think mmeshajulikana kama ni lazima mch** ndio mfunction, ili jambo lenu liende, nilitamani kumwambia Njomba Kimbulu ** maana mtakuwa mmekamilisha malengo yenu, kwa bahati mbaya Njomba hajawagundua ila mimi nawajua vizuri.”

Kiba ameendelea kuandika kuwa, “Sisumbuki tena, najua hata hiki nililichokiongea hapa kitawasaidia kwa sababu mimi ni KIng wenu, tena msije mkasema wa porono wakati wewe ndio wa porini. Tena mmekaa kikao kujadili na kurank wasanii, WHO ARE YOU?, nitaongea jambo lenu likiisha, haya sasa nadhani nime** vya kutosha tena kwa malengo mnayotaka, have a nice show.”

Ujumbe huo wa Kiba, umetafsiriwa kama dongo kwa mwimbaji Diamond na timu nzima ya WCB, Kufuatia yaliyojiri siku chache zilizopita kutoka kwa Sallam Sk na Babu Tale, kwa kuzingatia kuwa wao ndio wanaojiandaa na onyesho la funga mwaka linalotarajiwa kufanyika mwishoni mwa wiki hii jijini Dar es salaam.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live