Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Alikiba ana sumu ya Amapiano

Kiba Wazi Alikiba ana sumu ya Amapiano

Tue, 18 Jul 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mwaka mmoja tangu mwimbaji mkali wa muziki wa kizazi kipya nchini, Alikiba kukataa kuimba muziki wa amapiano, safari hii mambo yamemshinda mkali huyo wa mashairi ya mapenzi baada ya kuachia ngoma mpya ya miondoko hiyo iitwayo Sumu.

Kabla ya kuachia ngoma hiyo, Alikiba alihojiwa mwaka jana na kituo kimoja cha redio akisema hawezi kuimba katika miondoko hiyo, lakini juzi mkali huyo aliachia kazi hiyo mpya akishirikiana na Marioo.

"Kazi yangu ni muziki na sanaa ninayoifanya huwa naandika nyimbo kutokana na mzuka nilionao muda huo baada ya maombi mengi ya muziki wa Amapiano nafurahi kuachia kazi ya aina hiyo na imepokelewa vizuri." alisema Kiba anayetamba na kazi mbalimbali za muziki zikiwamo On Fire, Utu, Mwana, Mshumaa, Dodo, Ndombolo na Aje.

Miondoko hiyo ya Ampiano ambayo asili yake ni Afrika Kusini umejipatuia umaarufu nchini kutokana na wasanii karibu wote kuupiga, akiwamo Diamond, Marioo, Harmonize, Rayvanny, Zuchu, Nandy, Whozu, Mbosso, Damian Soul na wengineo.

Hata hivyo pamoja na wasanii wengi kushobokea miondoko hiyo ikiigwa pia hadi na waimbaji kutoka Nigeria, lakini kwenye tuzo za muziki za Afrika Kusini zilizofanyika April mwaka huu hakuna msanii hata mmoja wa Tanzania aliyeteuliwa kulinganisha na wenzao wa Nigeria.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live