Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Alikiba ampa pole Davido

Kiba Davido Mmm Alikiba ampa pole Davido

Wed, 2 Nov 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Staa wa muziki wa Bongo Fleva, Alikiba ameungana na mastaa wenzake kumpa pole msanii mwenzao, Davido kutoka Nigera ambaye amepata pigo kwa kuondokewa na mwanaye kipenzi anayefahamika kwa jina la Ifeanyi.

Ifeanyi alifariki alifariki dunia baada ya kuzama kwenye swimming pool wakati akiogelea nyumbani kwao, Oktoba 30, 2022.

Baada ya tukio hilo wasanii wengi na watu maarufu walimpa pole @davido mfano @harmonize_tz kutoka Tanzania na wengine.

Leo kupitia ukurasa wa Twitter wa @officialalikiba amempa pole @davido kwa kufiwa na mtoto wake.

@officialalikiba ameandika ujumbe kupitia Twitter wa kumpa pole; "The heaviest coffins are the small ones. May Allah give all the strength to @davido and his family. Being a father is an unexplainable blessing and losing a child is an unbearable pain that no one should ever experience in their lives," ameandika Kiba.

Taarifa za Polisi kutoka Lagos zilithibitisha kifo hicho na kueleza kuwa wamewakamata wafanyakazi 8 wa @davido kwa ajili ya mahojiano zaidi.

Siku ya leo Taarifa zimetoka kuwa kati ya hao 8 waliokatwa wafanyakazi 6 wameavhiliwa.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live