Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Alikiba amjibu shombo shabiki aliyemuulizia Amina

Ujumbe Wa Kiba Kwa Mkewe; 'Mungu Akupe Hitaji La Moyo' Alikiba amjibu shombo shabiki aliyemuulizia Amina

Thu, 7 Sep 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Alikiba wa siku hizi ni mtu mweye kuchangamka sana na kuwajibu mashabiki majibu yanayotupwa upande wake, kinyume za siku za nyuma ambapo msanii huyo alikuwa mhafidhina sana katika suala la kupakia au kutweet.

Msanii huyo hasa amekuwa akiteka anga katika mtandao wa X, awali ukiwa unaitwa Twitter ambapo juzikati alikuwa anampigia debe produsa wa wimbo wake mpya, Abbah akimsifia kwa kuutendea haki wimbo wake wa Huku – aliomshirikisha msanii wake Tommy Flavor.

Hapo ndipo shabiki mmoja alikurupuka na kutaka kujua mkewe Amina yupoje lakini Alikiba alimjibu kwa kumtuma kusikiliza wimbo wake wa Sumu aliomshirikisha Marioo wimbo wenye maudhui ya kutoa onyo kwa watu kukaa mbali na wachumba wa watu.

“Oyaa king nipo na swali la msingi why unadharau sana mzee? Swali dogo la nyongeza amina hajambo?” shabiki huyo alimuuliza.

“Swali la kwanza, Mwanangu nimewahi kuudharau wapi, kuhusiana na suala la pili, kasikilize wimbo unaitwa Sumu,” Alikiba alimjibu.

Kwa jibu hilo, Alikiba alikuwa anaashiria kumzima shabiki huyo ambaye anafuatilia mambo ya mkewe akimshauri kwamba mambo ya kufuatilia mke wa mtu hayafai, ni sumu.

Alikiba na Amina wamekuwa wakiparurana katika miezi ya hivi karibuni kuhusiana na suala zima la kutaka talaka.

Amina aliwahi kwenda moja kwa moja kwenye mitandao yake ya kijamii na kulalama vikali kwamba Alikiba amekuwa akimkomalia kwa kumnyima talaka licha ya yeye mwenyewe kuweka wazi kwamba hisia za kimapenzi kwa Alikiba sasa tena basi.

Amina katika ujumbe mrefu alimtaka Alikiba kukubali kumuandikia talaka yake ili kumweka huru kuliko kumfunga kwenye ndoa hali ya kuwa hana mapenzi naye tena.

Alikiba hajawahi zungumzia suala hilo moja kwa moja wakati anaulizwa na waandishi wa habari za mitandaoni.

Kwa wakati mmoja akiwa jijini Nairobi, aliulizwa na alisema kwamba hawezi kubabaishwa na jambo ambalo anajua fika jawabu lake – akiashiria kwamba suala la kumuacha mkewe kwa talaka ni dogo na anajua jinsi ya kulisuluhisha kabla ya kufikia hatua ya mwisho kabisa ya kutoa talaka.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live