Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Alikiba amefuata pesa Simba? Sikia majibu yake

Kiba Simba SC Alikiba

Sun, 6 Aug 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mapema leo hii wakati staa wa muziki na CEO wa lebo ya Kings Music Alikiba anarejea kutoka Mwannza kwenye show yake aliyoifanya usiku wa jana amekutana na wanahabari latika Uwanaja wa Ndege wa zkimataifa wa Julius Nyerere na kuongea naye mawili matatu.

Waandishi wamemuuliza Alikiba kuhusu siku ya leo ambayo ni Siku maalum ya Klabu ya ya Simba na yeye amejiunga na familia ya Simba akitokea Yanga, anawaahidi nini mashabiki wa Simba wakati yeye ndiye msanii mkubwa wa Kutumbuiza katika Tamasha hilo kwenye Dimba la Taifa?

Alikiba ameeleza namna alivyojipanga lakini vipi kuhusu mashabiki wanaodai eti yeye shabiki wa Yanga na simba amefuata hela?

Alikiba amejibu kuwa Bindamu hanunuliwi na yeye ameenda sehemu ambayo inamthamini, ameongeza kuwa amekutana na upendo wa tofauti sana kutoka kwa Wana Simba na kuahidi kuwa kamwe hatowaangusha.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live