Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Alikiba afunguka bifu la Marioo, Abby Chams

Marioo, Alikiba Na Abby Chams Alikiba afunguka bifu la Marioo, Abby Chams

Thu, 31 Aug 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mfalme Alikiba amezungumzia bifu linalotokota mjini kati ya Marioo na Abby Chams ambapo amewashauri wawili hao kama wadogo zake.

Kiba ametoa ushauri huo usiku wa kuamkia leo Agosti 31, 2023 pande za Zanzibar alipokuwa amekwenda kupafomu kwenye tamasha la Kizimkazi na ndipo alipozungumza na waandishi mara baada ya kupafomu.

"Ninachoweza kuwashauri kwa Marioo amuache tu yule ni mdogo wake na ni mtoto wa kike, asijibishane naye amuache tu. Kwa Abby yeye anatakiwa kuheshimu wakubwa zake, hata kama mtu amekuzidi umri kidogo unatakiwa kumuheshimu, sikuona sababu hata yeye kuuachia ule wimbo manake naona kama wanataka tu kushindana," alisema Alikiba.

Abby na Marioo waliingia kwenye vita ya maneno baada ya wawili hao kutuhumiana kuenguana kwenye wimbo waliorekodi pamoja studio unaokwenda kwa jina la Love Song.

Inasemekana Marioo aliamua kuachana na Abby wakiwa wamesharekodi wimbo huo na kuamua kumshirikisha Alikiba baada ya mrembo huyo kudai kuwa wimbo huo hajapendezwa nao lakini baada ya Marioo kuuachia aliofanya na Kiba ndipo Abby akaanza kulalamika kupitia Mange Kimambi.

Mange alisema, Marioo alimtoa Abby baada ya kushauriwa na mpenzi wake Paula na ndipo Marioo naye alipojibu mapigo kwa kutotaka inshu hiyo ahusishwe mpenzi wake.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live