Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Alikiba: Diamond akipata vazi ambalo natakiwa kuvaa tunafanya kolabo

Kiba Diamond .jpeg Diamond Platnumz na Alikiba

Sat, 20 Aug 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Miaka minane iliyopita kabla uhasama wa kimuziki kati ya Diamond Platnumz na Alikiba kukolea kwenye muziki, Alikiba aliwahi jibu baadhi ya maswali ya waandishi wa habari kuhusiana na kolabo yake na Diamond.

Majibu yake yakawapa bashasha mashabiki ambao walikuwa wakisubiri hata japo robo ya matumaini ya kujua kama kuna uwezekano wa King Kiba na Diamond kufanya kolabo.

August 20,2014 kwenye kipindi cha Jahazi cha Clouds Fm, Alikiba aliweka maneno, akitoa sababu zitakazopelekea afanye kolabo na Diamond.

“Mawazo ya kolabo yapo, mawazo unapata mengi tu, hiyo nimeshayasikia vilevile, na wewe sio mtu wa kwanza kuniuliza, hicho kitu kipo.

"Lakini muziki vile vile kama unavyoona kuna mavazi na style, vazi hili linatakiwa liende disko hili ni vazi la beach, vazi hili la ofisini, vazi hili la mpirani, hili la mchangani, hili la kwenye ukumbi unajua vitu kama hivyo! 

"Kwahiyo Diamond akipata vazi lake ambalo linahusiana na vazi ambalo natakiwa nivae, hakuna tatizo tunafanya kazi kama kawaida, kwa sababu yeye anafanya kazi vizuri,” AliKiba.

Bahati mbaya ni kuwa hadi hii leo August 20, 2022, Diamond hajapata vazi ambalo Alikiba anaweza kulivaa, yani Diamond bado hana muziki ambao Alikiba anaweza akaufeel na kumfanya aimbe naye.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live