Mwaka 1944 huko South Carolina mtoto wa miaka 14 aliyefahamika kwa jina la George Stinney Jr alikuwa binadamu mwenye umri mdogo zaidi kuhukumiwa kifo katika karne ya 20.
George aliuawa akiwa kwenye kiti cha umeme akiwa amevalishwa kichwani mkanda wa chuma wenye kupitisha umeme wa volti 5,380.
Kijana huyu alishtakiwa kwa kuua wasichana wawili wa kizungu, Betty wa miaka 11 na Mary wa miaka 7, ambao miili yao ilikutwa karibu na nyumba ambayo kijana huyo alikuwa akiishi na wazazi wake.
Wakati wa kesi yake, kila mara alikuwa akibeba Biblia mikononi mwake, akidai kuwa hana hatia.
Miaka 70 baadaye, mahakama ya huko South Carolina ilikuja kuthibitisha kuwa mtoto George hakuwa na hatia katika kesi hiyo iliyosababisha kifo chake.
Ikaelezwa kuwa mauaji hayo yalipangwa mtu mwingine na kumsingia George kwa kuwa alikuwa ni mtu mwesi.