Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Alichosema Shetta mwanaye kushinda Mwenyekiti Chipukizi

Alichosema Shetta Mwanaye Kushinda Mwenyekiti Chipukizi.jpeg Alichosema Shetta mwanaye kushinda Mwenyekiti Chipukizi

Thu, 21 Dec 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mwanamuziki wa Bongo Fleva, Shetta ameweka wazi kuwa mtoto wake Qayllah ambaye jana amechaguliwa kuwa Mwenyekiti wa Chipukizi CCM Taifa hakupata uongozi huo ghafla, alianza kuipenda CCM tangu akiwa na miaka mitatu.

Kupitia ukurasa wake wa Instagram msanii huyo ali-post video ikimuonesha Qayllah akiwa na umri wa miaka mitatu akiimba wimbo wa CCM, huku akiandika ujumbe usemao mtoto wake hajawa kiongozi ghafla, bali chama kilimuandaa tangu akiwa mdogo.

Qayllah amechaguliwa kuwa Mwenyekiti wa Chipukizi CCM Taifa baada ya kupata ushindi katika Mkutano Mkuu wa Chipukizi Taifa uliofanyika Disemba 20, 2023 kwa kupata kura 303.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live