Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Alichokisema mchumba wa MC Pilipili baada ya mwenzake kulia

35280 Pic+pili Alichokisema mchumba wa MC Pilipili baada ya mwenzake kulia

Wed, 9 Jan 2019 Chanzo: mwananchi.co.tz

Dar es Salaam. Philomena Thadey ‘Qute Menna’, mchumba wa mchekeshaji maarufu Emmanuel Mathias ‘MC Pilipili’ amesema hakujua kama mwenzake alikuwa analia wakati akimvalisha pete ya uchumba.

Menna ametoa kauli hiyo leo Jumatatu Januari 7, 2019 wakati akizungumza na Mwananchi kuhusu tukio la MC Pilipili kumwaga chozi wakati akimvisha pete, kitendo ambacho kimezua mjadala katika mitandao mbalimbali ya kijamii.

“Mwanzoni nilijua anafanya utani ndio maana sikujishughulisha kumtazama, nikisubiri atanyanyuka lakini  nikaona hanyanyuki na nilipomtazama vizuri nikabaini kuwa analia ndipo nikainama na kumtaka asilie,” amesema Menna.

“Nilichojifunza yupo hivyo yaani ni mtu wa emotion (hisia) sana, hawezi kujizuia kulia.”

Menna amesema kuwa kwa hali hiyo hata yeye alikuwa na taharuki ndio maana hakulia, kwa sababu hakuamini kama jambo lile lingetokea pale, alijua ni utani.

Menna ameeleza kuwa licha ya kuwa karibu na MC Pilipili kwa miezi minane, amempenda kwa sababu maisha yake yana msingi na mambo ya Mungu na ana upendo sana kwa watu wote.

MC Pilipili amesema alilia kwa sababu ilikuwa vita kubwa watu wakimwambia maneno mabaya kuhusu mchumba wake na ndoa kwa ujumla na machozi yake yalikuwa ya furaha.

“Yalikuwa ni mapambano makali wakati tukiwa wapenzi, watu walisema mengi ikiwamo waliolalama kuwa nimewanyang’anya mwanamke wao, ilikuwa kama nimekimbia na nimefikia fainali kwa hiyo yalikuwa machozi ya furaha, ”amesema Pilipili.

Pilipili  ameeleza kuwa pamoja na kumvisha pete Minna pia amemtolea mahari.

“Mahari ni Sh8 milioni, nimelipa Sh5 milioni nadaiwa Sh3 milioni, ndoa yetu itakuwa baada ya kupokea ujio wa Kristo yaani baada ya Pasaka sihitaji kupoteza muda hata kidogo, ”amesema Pilipili.

Amesema kuwa alipata wazo la kuoa baada ya kupata ajali mwaka 2018, “Mchumba wangu nilimuona harusini, ilikuwa sherehe ya mjomba wake na mimi nilikuwa msherekeshaji na yeye alikuwa miongoni mwa wasimamizi.”

“Pale pale likanijia wazo kuwa huyu ndiyo atakuwa mke wangu na mama wa watoto wangu, kila nikimtizama moyo ulikuwa unanienda mbio kutokea hapo hadi nimemvisha pete ya uchumba.”



Chanzo: mwananchi.co.tz