Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Alichokisema Wenger kuondoka kwa Giroud na ujio wa Aubameyang

Mon, 29 Jan 2018 Chanzo: bongo5.com

Meneja wa the Gunners, Arsene Wenger mwishoni mwa juma hili lililopita amesema kuwa mchezaji wake, Giroud kamwe hatoondoka hadi pale atakapo kuja mwingine ndani ya timu hiyo.



Hayo yanakuja wakati huu ambao klabu ya Arsenal inakaribia kumsajili, Pierre-Emerick Aubameyang kwa dau la paundi milioni 60 kutokea Borussia Dortmund.

Inafahamika kuwa mazungumzo yanaendelea baina ya pande zote mbili na dili bado halijafika mwisho kuweza kumnasa straika huyo.

Arsenal mpaka sasa imefikia kiasi cha paundi milioni 50 wakati klabu ya Dortmund ikiwa chini ya muongozaji mkuu wa timu hiyo, Michael Zorc amesema kuwa ili kumuachia mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 28 watalazimika kutoa kitita cha paundi milioni 60.

 

Chanzo: bongo5.com