Dar es Salaam. Kama ni mfuatiliaji wa burudani hakika utakuwa umekumbana na mjadala kuhusu kuhusu Sallam SK ambaye ni meneja wa Diamond Platnumz kuacha kumsimamia mkali huyo wa wimbo wa Jeje.
Mjadala huo ulitokana na Sallam kubadili baadhi ya taarifa zake katika ukurasa wa mtandao wake wa kijamii wa Instagram.
Awali, aliandika kuwa ni meneja wa Diamond huku akitaka watu wanaotaka kuwasiliana na msanii huyo waanzie kwake.
Jana Ijumaa Aprili 3, 2020, Sallam alibadili maelezo hayo na kujitambulisha kuwa ni mfanyabiashara, jambo lililoibua mjadala mitandaoni huku baadhi ya wachangiaji wakidai huenda amejiengua katika lebo ya Wasafi.
Leo Jumamosi Aprili 4, 2020 katika ukurasa huo, Sallam ameweka picha akiwa na Diamond na kuandika, “umewaona wale wanataka kuboost viblog vyao vimekosa habari. Sasa wacha tuwape habari njema au unasemaje Diamond, wajiandae leo au kesho.”
Diamond naye alijibu ujumbe huo kwa kuandika, “nakusikiliza mzee Prodesa, wee nipe su, nisusushe.”
Pia Soma
- Ndani ya Boksi: Darassa mpaka ale unga ili tumuelewe?
- DJ SinyorRita ajivunia kuwa na fani ya kipekee
- Mchumba wa Davido akutwa na maambukizi ya corona
Baadhi ya watu waliotoa maoni yao kuhusu ujumbe huo akiwemo Sells Beats amesema "achia ngoma mpya watu wapo lock down, wanatakiwa wakatazame video nzuri YouTube.”
IQ Msafi, amesema “mtakoma mliojifanya mnatusimulia ya Sallam na Diamond.”