Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Alichoitiwa Baba Levo Basata hiki hapa

Basata Pic Data Alichoitiwa Baba Levo Basata hiki hapa

Thu, 15 Apr 2021 Chanzo: www.mwanaspoti.co.tz

Imeelezwa kuwa moja ya sababu ya kuitwa kwa  Msanii Baba Levo, ni wimbo wake wa 'Harmo Ma**', aliouachia juzi usiku.

Baba Levo alifika Basta leo Alhamisi Aprili 15, 2021, kwa ajili ya kuitikia wito baada ya kutakiwa kufanya hivyo jana na mmoja wa maofisa wa Basata.

Hata hivyo habari za ndani ambazo Mwananchi imezipata ni kwamba moja ya sababu ya kuitwa kwake ni pamoja naa wimbo wake huo wa Harmo Ma**.

Ndani ya wimbo huo mashairi yake ni kama yanaeleza sakata linaloendelea kati ya Rayvanny na Harmonize ambapo tayari wasanii mbalimbali wameonekana kudandia ugomvi huo akiwemo Ibra kutoka Konde Gang, lebo anayomiliki Harmonize na Dulla Makabika msanii wa singeli ambaye yupo karibu sana na familia ya wasafi.

Mnyetishaji habari huyo pia amesema kingine alichoitiwa Baba Levo ni pamoja na kuwepo kwa malalamiko kutoka kwa watu mbalimbali wakiwemo wasanii wenzake ambao wanadai amekuwa akiwachafua majina yao huku wengine wakiwa ni mabalozi wa huduma na bidhaa mbalimbali hali inayotishia kufutwa ubalozi wao

Chanzo: www.mwanaspoti.co.tz