Trending kwenye Instagram ipo pia picha ya mtoto wa Billnass na Nandy ambaye kwa mara ya kwanza, wamemuonesha sura na kumuachia picha yake mitandaoni.
Kupitia Instagram, Billnass ameposti picha akiwa amembeba mwanaye huyo na kusindikiza na ujumbe huu kumtakia lakheri katika mwaka wake mmoja wa kuzaliwa:
"Kwa Majaliwa na baraka zake Mungu amekufanya uwe katika uzao wangu… @naya_bill Mimi na Mama Yako tunakupenda sana, Na Ujio wako umeleta Furaha na Kuimarisha upendo Katika Familia Yetu!! Umetimiza Mwaka Sasa, Sina Budi Kukupost ili Uwe Huru unaposafiri,Unapohudhuria Kanisani, Clinic na Kwenye mambo yote ya kijamii…una kila sababu ya kuufurahia ulimwengu na Namuomba Mungu akuongoze ili siku moja ulimwengu ufurahie uwepo wako katika Ulimwengu