Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Ali kiba ajiweka pembeni Coastal Union

20033 Pic+alikiba TanzaniaWeb

Mon, 1 Oct 2018 Chanzo: mwananchi.co.tz

NYOTA wa muziki wa kizazi kipya ambaye hivi sasa amegeukia kwenye soka Ally Saleh ‘Alikiba’, amesema yeye binafsi ndio amemuomba kocha wa Coastal Union asicheze ili ajiimarishe zaidi.

Alikiba ameyasema hayo juzi Ijumaa mara baada ya kushindwa kuonekana kwenye mchezo wa saba wa timu yake ambayo imelazimishwa sare ya bao 1-1 na Mbao FC kwenye uwanja wake wa nyumbani wa Mkwakwani jijini Tanga.

‘’Nafanya mazoezi kabla ya kucheza ili nikianza watu wajue kweli Alikiba ni mchezaji na sio kwamba nimekuja kujifurahisha, nimemwomba kocha wangu Juma Mgunda na amenielewa” alisema.

Alikiba ameeleza kuwa kitu kikubwa kilichomfanya asionekane kwenye mechi saba za kwanza za Ligi Kuu msimu huu, ambazo Costal Union imecheza ni kutaka kuzoeana na wenzake ili kutengeneza muunganiko uwanjani.

Coastal ambayo imerejea Ligi Kuu msimu huu baada ya kushuka mwaka 2016, mpaka sasa ina alama 10, ikiwa katika nafasi ya 7 kwenye msimamo wa ligi ambayo ina jumla ya timu 20iliposhuka ilikuwa na timu 16.

Chanzo: mwananchi.co.tz