Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Ali Kiba kuisimamisha Kigoma

B56b4a162d0201ea5a841c58c5b7784d Ali Kiba kuisimamisha Kigoma

Fri, 14 Aug 2020 Chanzo: habarileo.co.tz

MSANII wa muziki wa kizazi kipya, Ali Kiba, leo anatarajiwa kufanya onesho katika Uwanja wa Lake Tanganyika, mjini Kigoma.

Kiba ambaye atasindikizwa na wasanii kibao katika tamasha hilo linaloitwa ‘Home coming concert’, amewashukuru wakazi wa Kigoma kwa mapokezi makubwa waliyompatia alipofika mjini humo jana kwa treni.

Baada ya msanii huyo kuwasili Kigoma, mji ulisimama kwa saa kadhaa kupisha mapokezi yake na wasanii wenzake kama Marioo, Bill Nass, Tommy Flavour, Abdu Kiba na Abby Skillz, ambapo mashabiki waliwasindikiza mpaka hotelini walipofikia.

“Asanteni ndugu zangu Kigoma, wahi kuchukua tiketi yako mapema kwa Sh 5,000 tu kawaida na kwa VIP Sh 20,000. Milango itakuwa wazi kuanzia saa 10:00 jioni, uwanjani kutafungwa Tv kubwa kwa ajili ya kuangalia mechi ya Ligi ya Mabingwa Ulaya kati ya PSG na Barcelona, baada ya hapo shughuli itaendelea mpaka asubuhi.”

“Ni kama filamu, lakini ni kweli Kigoma, Omukwano tutaipiga live, nikiwa na kijana wangu Tommy flavour Lake Tanganyika,” aliandika Kiba kwenye ukurasa wake wa Instagram jana.

Awali, tamasha hili lilipangwa kufanyika mwezi uliopita, lakini liliahirishwa kutokana na maombolezo ya kifo cha Rais wa Awamu ya Tatu, Benjamin Mkapa.

Chanzo: habarileo.co.tz