Lifestyle

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

SIL

Ali Kiba amlilia Malcolm

3440c054fbedab9ea515aef0672080be.jpeg Ali Kiba amlilia Malcolm

Fri, 30 Jul 2021 Chanzo: www.habarileo.co.tz

MSANII mkongwe wa muziki wa kizazi kipya Ali Kiba ameguswa na kifo cha mtoto wa Mtangazaji maarufu wa Clouds Media Masoud Kipanya, Malcolm Masoud aliyefariki dunia janai.

Kijana huyo (20) aliyekuwa akisumbuliwa na ugonjwa wa kudhoofisha misuli na viungo kwa muda mrefu anatarajiwa kuzikwa katika makaburi ya Kisutu Dar es Salaam leo.

Kiba kupitia ukurasa wake wa mtandao wa kijamii wa Instagram aliandika ujumbe kuonesha namna alivyoguswa na kifo cha Malcolm.

“Nimepokea kwa masikitiko makubwa taarifa za kifo cha rafiki yangu Malcolm Masoud, mtoto wa kaka yangu Masoud Kipanya, Allah amuweke mahali pema peponi, awape uvumilivu na imani familia yake,”aliandika.

Enzi za uhai wake Malcolm aliwahi kuandika ujumbe akielezea namna alivyoteseka na ugonjwa huo tangu akiwa kijana mdogo wa umri wa miaka tisa huku akijipa moyo na kutoa maneno ya faraja kwa watu mbalimbali wenye matatizo kama yake.

Alitaja chanzo cha ugonjwa wake ulitokana na kuvunjika miguu yote miwili ambapo wa kushoto ulivunjika katikati na kulia katikati na kwenye goti na kuanzia hapo hakuweza kutembea tena zaidi ya kuishi kwa mateso hadi umauti ulipomfikia.

Licha ya kuishi na ugonjwa huo kwa muda mrefu Baba wa mtoto huyo, Kipanya alitaja chanzo cha kifo cha kijana wake, alianza kuumwa kikohozi na homa jana na baada ya kufanyiwa vipimo alibainika mapafu yamejaa maji na baadaye alizidiwa na kufariki akiwa njiani kupelekwa Hospitali ya Taifa ya Muhimbili.

Chanzo: www.habarileo.co.tz