Sherehe ya Abdi Banda na Zabibu Kiba imefanyika jana Jumamosi usiku kwenye Ukumbi wa Beach Resort jijini Tanga.
Msanii Ali Kiba hakuwa mbali kwa alionekana akimsaidia mdogo wake Zabibu Kiba kutambulisha familia baada ya Zabibu kushindwa kumalizia utambulisho baada ya kushikwa na furaha iliyomfanya kuangua kilio.
Katika sherehe hiyo, Waziri wa Afya,Jinsia, Maendeleo ya Jamii na watoto, Ummy Mwalimu alinogesha baada ya kucheza kwa madaha, huku akimuongoza kuingia ukumbini mama wa Abdi Banda.
Familia ya Zabibu Kiba iliingia ukumbini kwa shangwe na kupokewa na wazazi wenzao kwenye ukumbi huo huku watu waliokuwepo ukumbini hapo wakishangilia.
Abdi Banda na mkewe Zabibu Kiba walionyesha ufundi wa kucheza baada ya kupewa nafasi hiyo ambapo nyota huyo wa soka alionyesha umahiri wa kusakata muziki huku akipokeana na mkewe Zabibu.