Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Ali Kiba, Harmonize jukwaa moja tamasha la Fiesta

86008 Pic+fiesta Ali Kiba, Harmonize jukwaa moja tamasha la Fiesta

Thu, 28 Nov 2019 Chanzo: mwananchi.co.tz

Dar es Salaam. Wasanii wa Tanzania,  Alikiba na Harmonize watakutana katika jukwaa moja la tamasha la Fiesta  litakalofanyika katika uwanja wa  Uhuru jijini Dar es Salaam Desemba 8, 2019.

Waandaaji wa tamasha hilo leo Jumanne Novemba 26, 2019  wametangaza  baadhi ya wasanii  nchini watakaoshiriki Fiesta, wakiwemo wawili hao.

Kukutana jukwaani kwa wasanii hao kunasubiriwa kwa hamu kutokana na Harmonize kuachana na lebo ya Wasafi, hivyo mashabiki wengi kutaka kumshuhudia akitoa burudani nje ya lebo hiyo.

Alhamisi ya Oktoba 24, 2019, Harmonize alieleza jinsi alivyouza nyumba zake tatu na baadhi ya mali ili kuilipa lebo ya Wasafi Sh500 milioni kwa ajili ya kupata hakimiliki ya kutumia nyimbo zake na jina.

Alibainisha kuwa mkataba alioingia na lebo ya Wasafi inayomilikiwa na msanii Diamond Platnumz ilikuwa na kipengele cha kulipa kiasi hicho cha fedha ikiwa atavunja mkataba ili aweze kuendelea kutumia nyimbo pamoja na jina lake la kisanii.

Wakati akiwa Wasafi, Harmonize hakuwahi kushiriki tamasha la Fiesta tofauti na Ali Kiba aliyewahi kushiriki mara kadhaa.

Chanzo: mwananchi.co.tz