Baraza la Sanaa la Taifa ‘BASATA’ limewapongeza wasanii ambao wamekuwa wakifuata kanuni zilizowekwa ikiwemo kuchukua vibali wanapoenda kufanya matamasha nje ya nchi na wale wanaochukua vibali kwa ajili ya matamasha ya burudani yanayofanyika hapa nchini, hlo limekja kufuatua zoezi la lililofanyika hivi karibuni ambapo araza litatoa vyeti vya pongezi kwa wasanii na waandaaji wa matamasha ambao wanafanya vizuri.
Pongezi hizo zimetolewa na Katibu Mtendaji wa Baraza la Sanaa la Taifa ‘BASATA’ Dkt. Kedmon Mapana ambapo amesema sheria inawataka wasanii kupata vibali wanapofanya shughuli zao, ambapo kwa mwaka 2023, baraza hilo limefikia uamuzi wa kutoa mfano kwa kuwapongeza na baadae vitatolewa vyeti vya pongezi kwa wasanii waliofanya vizuri katika kufuata sheria na kanuni zilizowekwa.
Dkt Mapana amebainishwa kuwa wapo wasanii ambao kwa mwaka 2023 wamefanya shughuli zao nje ya nchi lakini pia wameongoza kwakufanya vizuri kwakufuata sheria ambapo walioongoza kwa upande wa wasanii wa sarakasi ni Fadhil Ramadhan Rashid (Ramadhan Brothers), wakifuatiwa na kundi la Dj aliyefanya vizuri Hamadi Hassan Mbelwa maarufu kwa jina la Dj Travella.
Akizungumza kuhusu Wasanii wa muziki wa Bongo fleva Tanzania amesema msanii aliyeongoza ni Naseeb Abdul maarufu Diamond Platnum, akifuatiwa na Ally Salehe maarufu Ally Kiba, na kwa upande wa maeneo ya burudani yaliyoongoza kwa kuomba vibali vya kuingiza wasanii ametaja Club Element wakifuatiwa na 1245 Lounge Bar and Restaurant na Mapromota waliofanya vizuri ni Food and Bevarege Master Limited wakifuatiwa na sinech consept limites.