Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Ali Choki arejea kwa kishindo na Extra Bongo

Chokiii Ali Choki arejea kwa kishindo na Extra Bongo

Tue, 21 Nov 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mwanamuziki mkongwe wa muziki wa dansi nchini, Ali Choki ‘Kamarade’ ukipenda Mzee wa Farasi leo ameibuka tena na Bendi yake ya Extra Bongo sasa hivi akiinogesha na jina la Baba Lao ambapo mwanamuziki huyo amesema anakuja na nyimbo kibao ikiwemo Penati ya Mwisho na nyinginezo na sasa hakuna kulala tena ni mwendo mdundo mpaka kieleweke.

Ali Choki ambaye miaka kadhaa iliyopita aliamua kuivunja bendi hiyo na kujhihusisha na mambo yake mengine sasa amerudi tena na bendi hiyo ambapo amesema itafanya uzinduzi rasmi Desemba 2 mwaka huu kwenye Ukumbi wa Andrewson zamani ukiitwa T Garden uliopo Sinza Lion Jijini Dar.

Choki katika kuinogesha bendi hiyo sasa hivi atakuja na chipukizi wengi wenye mawazo ya kileo zaidi ili kuwateka vijana na kuchanganyia na wakongwe wachache kwa ajili ya kuchanganya radha.

Kiongozi mstaafu wa Chama cha Muziki wa Dansi nchini, (CHAMUDATA) Hassan Msumari akielezea furaha yake kufuatia kurudi upya kwa Extra Bongo Baba Lao.

Ameendelea kusema kuwa katika uzinduzi huo kiingilio kitakuwa shilingi elfu kumi kawaida na meza maalum yaani (VIP) itakayosheheni vinywaji, minofu na asusa mbalimbali itakuwa shilingi laki mbili. Mwanamuziki huyo amesema katika ujio wa bendi anatarajia kutamba na wimbo wa penati ya mwisho na nyinginezo ambazo anaamini zitawashika mashabiki.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live