Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

TV

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Algeria yapiga marufuku filamu ya Barbie kwa madai ya ukiukaji wa maadili

Algeria Yapiga Marufuku Filamu Ya Barbie Kwa Madai Ya Ukiukaji Wa Maadili Algeria yapiga marufuku filamu ya Barbie kwa madai ya ukiukaji wa maadili

Tue, 15 Aug 2023 Chanzo: Bbc

Algeria imepiga marufuku filamu ya Kimarekani ya Barbie, ambayo imekuwa ikioneshwa katika kumbi za sinema nchini humo kwa wiki kadhaa.

Mamlaka zinasema filamu hiyo, ambayo ilitolewa mwezi uliopita, inaenda kinyume na maadili ya Algeria.

Shirika la habari la Reuters lilinukuu chanzo rasmi kikisema kwamba filamu hiyo "inakuza mapenzi ya jinsia moja na upotovu mwingine wa Magharibi" na kwamba "haiendani na imani za kidini na kitamaduni za Algeria".

Filamu ya Barbie tayari imepita alama ya mabilioni ya dola baada ya utangulizi wake wa Julai 21. Baadhi ya nchi nyingine zikiwemo Lebanon na Kuwait zimepiga marufuku filamu hiyo kwa misingi ya maadili.

Chanzo: Bbc