Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Alenga ashangazwa na ‘Love or Money’

WhatsApp Image 2020 09 03 At 14.34.37.jpeg Alenga ashangazwa na ‘Love or Money’

Thu, 3 Sep 2020 Chanzo: mtanzania.co.tz

MWONGOZAJI na mwigizaji anayefanya vizuri, Houston, Texas, Marekani, Alenga Elize ‘Alenga The Great’, ameshangazwa na mapokezi makubwa ya filamu yake mpya, Love or Money.

Alenga The Great, ameliambia Papaso la Burudani kuwa filamu hiyo yenye ujumbe mzuri kuhusu nguvu ya mapenzi na pesa imetazamwa na watu wengi kwenye YouTube ndani ya muda mfupi.

“Nashukuru mapokezi yamekuwa makubwa, filamu hii tayari ipo kwenye chaneli yangu ya YouTube (Alenga The Great Films) ambapo ilitazamwa na watu 2,000 (2k) ndani ya saa 10, haya ni mafanikio makubwa kwangu na kwa wasanii nilioshirikiana nao,” alisema Alenga.

Chanzo: mtanzania.co.tz