Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Albamu ya Tyler yafanya maajabu Spotify

Tyla 110723 625bb93003a94fd7b88a64e11d58ae11 Mwanamuziki kutoka South Africa, Tyla

Tue, 4 Jun 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mwanamuziki kutoka South Africa ambaye alijulikana zaidi kupitia wimbo wake wa ‘Water’ Tyla ameendelea kufanya vizuri kupitia ngoma zake, hii ni baada ya albumu yake iitwayo ‘Tyla’ kufikisha zaidi ya wasikilizaji (streams) bilioni moja katika mtandao wa Spotify.

Albumu hiyo yenye ngoma 14 akiwashirikisha wasanii kama Gunna, Tems, TravisScott na wengineo iliachiwa rasmi Machi 22, 2024 huku ikichukua miezi miwili tu kufikisha wasikilizaji bilioni 1.

Haya siyo mafanikio ya kwanza kwa Album hiyo kwani imewahi kushika nafasi ya kwanza kwenye chati ya ‘Billboard World Album Chart’ wiki chache tangu kuachiwa kwake.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live