Kundi la muziki Bongo, Navy Kenzo linaloundwa na Aika na Nahreel linatarajia kuachia albamu yake ya tatu ‘Most People Want This’ Machi 9 mwaka huu.
Hadi sasa Navy Kenzo wametoa albamu mbili, Above Inna Minute (AIM) iliyotoka Desemba 2016 ikiwa na nyimbo 11, pia kuna Story Of The African Mob iliyotoka Septemba, 2020 ikiwa na nyimbo 12.
Tayari wimbo wa kwanza kutoka kwenye albamu hiyo, Don’t Let Go umetoka na unafanya vizuri.
Navy Kenzo watakuwa wasanii wa kwanza wa Bongofleva kuachia albamu mwaka huu baada ya mwishoni mwa mwaka jana wasanii kama Marioo na Jux kufanya hivyo.
Hatua hiyo ni baada ya kusikika kwenye albamu ‘Where we come from’ kupitia wimbo wao, Hold On walishirikiana na FireBoy DML wa Nigeria.
Albamu hiyo iliyotoka chini ya Empire, ilikutanisha wasanii wengine kama Olamide, Kizz Daniel, Buju BNXN, Asake na Black Sherif.