Baada ya miaka mitatu ya kifo cha aliyekuwa nguli wa Hip-Hop Marekani na Duniani Earl Simon wengi wa kimfahamu kama DMX sasa imetangazwa December 13 kama tarehe rasmi ya ujio wa Album yake mpya inayoitwa 'LET US PRAY CHAPTER X' Iliyotengenezwa chini ya producer Warryn Campell.
Album hii imekaa kiutukufu zaidi ikiwa na jumla ya ngoma nane, Gospel zikiwemo humo ndani pamoja na beats mbali mbali ambazo hazijawahi kufanyiwa kazi wala kuingizwa 'Vocals'.
DMX Album yake ya mwisho ilitengenezwa na mshikaji wake aliyekuwa rafiki yake wa karibu Swizz Beats iliyoitwa 'EXODUS'.
DMX alifariki April 2 2021, chanzo kikiwa ni 'Heart Attack' iliyopelekea moyo, mapafu, figo na ini kufeli.